Kamati ya utekelezaji ya UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatatu Juni 15,2020 imefanya ziara kuona maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya Comrade Dotto Joshua na Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Agnes Bashemu (Mtoto wa Mama).
Wajumbe kwa pamoja wamepongeza na maendeleo ya Ujenzi ambapo Ujenzi umefikia hatua nzuri ya ukamilishaji wa Boma la nyumba.
Kamati ya Utekelezaji kwa kauli moja, imetoa shukrani kwa wadau wote ambao wamekuwa bega kwa bega katika kuhakikisha Ujenzi unakamilika na kwamba Kamati inaendelea kuwaomba wadau Mbalimbali kuendelea kujitoa kwa moyo wa hali na mali ili kufanikisha Ujenzi wa Nyumba ya katibu UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini.
Sambamba na hivyo, Kamati ya utekelezaji imetoa pongezi za Dhati kwa Mwenyekiti UVCCM Taifa Comrade Kheri Denice James (MCC) Pamoja na Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa kwa Maono yao ya Kuhakikisha watendaji wa Jumuiya ya Umoja wa CCM wanakuwa na Makazi Bora na Uhakika
Imetolewa na Idara Ya Hamasa &Chipukizi
Peter Mgalula
Kamati ya utekelezaji ya UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakishiriki ujenzi wa nyumba ya katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini
Social Plugin