Jumla ya wanachama Milioni 1,023, 911 wa chama cha Mapinduzi, CCM wamejitokeza kumdhamini Mwenyekiti wao Rais Magufuli katika fomu za kuwania kupitishwa na chama hicho kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Hayo yameelezwa leo Jumanne tarehe 30 Juni 2020 makao makuu ya CCM, Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally wakati wa hafla fupi ya kuzipokea Fomu za Kugombea Urais wa Tanzania Zilizowasilishwa na Rais Magufuli
Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM, Serikali na wanachama wa chama hicho wakiwemo wenyeviti wa chama hicho nzima waliowasilisha kila mmoja fomu za udhamini.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa, Dk. Bashiru amesema, jumla ya wanachama Milioni 1,023, 911 walijitokeza kumdhamini Rais Magufuli kutoka mikoa 32 na jumuiya zake tatu za wazazi, vijana na wanawake.
Amesema, leo Jumanne saa 10 jioni ndiyo siku ya mwisho ya uchukuaji na urejeshaji fomu za urais ndani ya chama hicho. Aliyechukua ni mmoja tu ambaye ni Rais Magufuli.
Social Plugin