Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza kwenye mjadala wa Wadau wa Tasnia ya Maziwa yaliyokuwa mbashara kwa njia ya video-conference jijini Dodoma
Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt.Sophia Mlote,akitoa ufafanuzi jambo kwenye mjadala wa Wadau wa Tasnia ya Maziwa yaliyokuwa mbashara kwa njia ya video-conference jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na Ugani kutoka wizara ya mifugo Dkt.Angello Mwillawa akichagia mada kwenye mjadala wa Wadau wa Tasnia ya Maziwa yaliyokuwa mbashara kwa njia ya video-conference jijini Dodoma
Sehemu ya wadau wa maziwa wakiwa kwenye mjadala wa Wadau wa Tasnia ya Maziwa yaliyokuwa mbashara kwa njia ya video-conference jijini Dodoma
………………………………………………………………
Na. Mwandishi Wetu, Dodoma
Serikali imepanga kuendelea kuhamasisha uzalishaji wa maziwa kutoka lita bilioni 3.01 za sasa hadi kufikia bilioni saba ifikapo 2025.
Kauli hiyo imetolewa na KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, (Sekta ya Mifugo), Prof Elisante Ole Gabriel amesema kabla ya kuanza mjadala wa Wadau wa Tasnia ya Maziwa yaliyokuwa mbashara kwa njia ya video-conference.
Aidha Profesa Gabriel amesema kuwa uzalishaji kwa sasa umefikia lita 3.01 mwaka jana kutoka 2.7 mwaka juzi.
Profesa Gabriel amesema mkakati huo wa serikali utafanikiwa tu kama wazalishaji na wasindikaji watashiriki katika kuhamasisha umma, kuzalisha lakini unywaji wa maziwa utakaoenda sambamba na unywaji.
Katika mjadala huo unaolenga kukusanya maoni nini kifanyike ili uzalishaji maziwa uongeze tija, wadau kuhamasisha uzalishaji lakini pia kutafuta masoko ya maziwa yanayozalishwa.
Pia Wadau wameomba serikali kuongeza uwigo wa kutoa mikopo kwa wazalishaji kwa wazalishaji na wasindikizaji ili kuongeza usindikaji maziwa bora nchini.
Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dk Sofia Mlote amesema kuwa ili kuhakikisha maziwa yanayoingia sokoni yanakuwa bora, imekuwa ikikamata shehena ya maziwa yasiyofuata taratibu hasa Ubungo Dar es Salaam.
Dk. Mlote amesisitiza kuwa Bodi hiyo imekuwa ikifanya juhudi katika kutekeleza maziwa ambayo hayajafuata tarataribu pamoja na kuwatoza ffaini wanaoingiza maziwa hayo kutoka Kibaya, Morogoro na mahali pengine.
Naye Asha Lukaso kutoka Rungwe amesema kuwa ili kuongeza tija katika uzalishaji wa maziwa lazima kuangalia upya mfumo wa utoaji mikopo kwa wafugaji kwani imekuwa na riba kubwa.
Huku Bernard Manyamba kutoka Tandahima Mtwara ametoa wito kwa serikai kuhamasisha wafugaji kufuga kisasa ili kuwa na ng’ombe bora wa kutoa maziwa bora.
“Sasa ni wakati wa kuhamasisha wananchi kujenga viwanda vidogo vigodo kwa ajili ya usingikizaji wa mazira ambao utaenda sambambana ufugaji wa ngombe wa kisasa”, ameongeza Alfred Mgolole kutoka Tanga.
Kwa upande wake Restistuta Ndelwa kutoka Njombe amesema kuwa inatakiwa kutolewa elimu ya ufugaji pamoja na kuwafanya vijana waingie katika tasnia hiyo ambayo ina faida nyingi zikiwemo za ajira na tija kwa lengo la kuandaa miundombinuya ufugaji hasa vitendea kazi.
Innocent Mushi kutoka Kiwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh amesema kuna takiwa kuwa na mkakati wa vituo vya ukusanyaji maziwa ili wenye viwanda wafike hapo na kuchukua hivyo maziwa yanayozalishwa yatafika kusindikiwa.
Akizungumza Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dk Sofia Mlote amesema kuwa bodi imekuwa ikifanya juhudi katika kutekeleza maziwa ambayo hayajafuata tarataribu pamoja na kuwatoza faini wanaoingiza maziwa hayo kutoka Kibaha, Morogoro na mahali pengine.
Profesa Ole Gabriel amehitimisha kwa kusema kuwa katika uhamashishaji jamii kunywa maziwa, utatu wa wadau yaani serikali, wazalishaji na wasindikaji wanatakiwa kushirikiana katika kuhamasisha jamii.
“Wadau wanatakiwa kuendele kuhimiza unywaji wa maziwa hata kama kumekuwa na uongezeko kutoka lita 49 kwa mtu hadi lita 53.9 kwa mwaka 2019/20,”amesisitiza Profesa Gabriel.
Social Plugin