Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TICTS YAKABIDHI VIFAA VYA MILIONI 182/- KWA WIZARA YA AFYA, MGANGA MKUU WA SERIKLI ATOA SHUKRANI KWA SEKTA BINAFSI


Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Abel Makubi (wa pili kushoto) pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula (kushoto) wakiushukuru Uongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya kuhudumia Makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo,Horace Hui (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo wa TICTS, Donald Talawa kwa mchango wao wa kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh.milioni 182, ikiwa ni jitihada ya kuunga mkono Serikali katika sekta ya afya,Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya kuhudumia Makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Horace Hui (wa pili kulia) akizungumza na Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Abel Makubi (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vya kujikinga na ugonjwa wa Corona, vilivyotolewa na Kampuni hiyo, mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Kaimu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo wa TICTS, Donald Talawa. 
Baadhi ya vifaa Kampuni ya TICTS ilivikabidhi kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni vitanda 100 ,mashuka, mito, vitakasa mikono vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 182/- ambavyo serikali itapeleka katika vituo mbalimbali vya afya.
Picha ya pamoja
====== ========= ======== ===============

KAMPUNI ya Kimataifa ya kuhudumia Makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS),imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh.milioni 182, ikiwa ni jitihada ya kuunga mkono Serikali katika sekta ya afya .

Akizungumza mwishoni mwai wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi msaada huo, kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Mkurugenzi wa Uendeshaji Donald Talawa amesema kuwa TICTS ni sehemu ya watanzania, hivyo inawajibu wa kuunga mkono Serikali katika nyanja mbalimbali.

Talawa amesema kutokana na Serikali kuongeza vituo vya afya, kampuni hiyo imeona kuna umuhimu wa kusaidia vifaa mbalimbali vitavyosaidia vituo vya afya kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Talawa ametaja vifaa hivyo walivyokabidhi kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni vitanda 100 ,mashuka, mito, vitakasa mikono ambavyo serikali itapeleka katika vituo vya afya.

"TICTS ni kampuni binafsi katika Bandari ya Dar es Salaam hivyo ni sehemu ya watanzania wa kuweza kuhakikisha tunaunga jitihada za Serikali katika sekta ya afya kwa vifaa Kinfa na Tiba kutokana na kuongezeka kwa vituo vya afya nchi nzima,"amesema Talawa.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi ameishukuru TPSF kwa uratibu wao kwa sekta binafsi ikiwemo Kampuni ya TICTS kuchangia vifaa tiba hivyo ili vituo vya afya kuwa na vifaa muhimu vya kutolea huduma.

“Wizara ya afya pamoja na TAMISEMI kwa kipindi cha miaka mitano tumeimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa kinga,hivyo tunaishukuru sekta binafsi kwa kukubali kuchangia kwa umoja wenu katika jitihada za serikali ili vituo vya afya kuwa na vifaa tiba,”amesema.

Aidha, Prof. Makubi amesema kuwa Serikali inahakikisha vituo vya kutolea huduma za afya nchini vinakuwa na vifaa muhimu vya kutolea huduma na huduma bora zinazotolewa kwa wananchi pamoja na huduma zipatazo 13 za kipaumbele ikiwemo huduma za mama na mtoto kwa kupunguzavifo vya mama na mtoto.

"Sisi kama watumishi wenu tunathamini michango yenu,kwakweli mmefanya kazi kubwa".

Prof. Makubi ameongeza kwamba kwa kipindi cha miaka mitano Serikali imeongeza vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 7014 hadi 8783 ambapo kuna ongezeko la vituo 1769 zikiwemo zahanati 1198 na vituo vya afya 487 na hivyo wataendelea kuimarisha upatikanaji wa vitaa tiba na dawa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com