Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango amesema kuwa ukuaji wa pato halisi la Taifa unatarajiwa kupungua kutoka maoteo ya awali ya asilimia 6.9 na kufikia asilimia 5.5 mwaka 2020 ikilinganishwa asilimia 7.0 mwaka 2019.
Akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2020/2021 bungeni jijini Dodoma, Waziri Mpango amesema kuwa hali hiyo inatokana na athari za ugonjwa wa corona ulioenea katika nchi mbalimbali duniani ambazo ni washirika wakubwa wa Tanzania kibiashara.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2021, serikali itaendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki katika wigo wa tarakimu moja kati ya wastani wa asilimia tatu hadi tano.
Kwa mujibu wa Waziri Mpango, kwa mwaka 2020/2021 mapato ya ndani yanatarajiwa kufikia asilimia 14.7 ya Pato la Taifa kutoka matarajio ya asilimia 14.0 mwaka 2019/2020 huku matumizi ya serikali yakitarajiwa kuwa asilimia 22.1 ya pato la Taifa mwaka 2020/2021.
Social Plugin