Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwafukuza kazi wafanyakazi wa shirika hilo wanaowatoza fedha na wanaochelewesha zoezi Kutoa nembo ya ubora kwa bidhaa zinazotengenezwa kwenye Viwanda vidogo nchini.
Waziri Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo 30 juni 2020 alipofanya ziara mkoani Simiyu na kutembelea kiwanda cha Usindikani wa Viazi lishe kilichopo wilaya ya Maswa kinachojulikana kwa jina la Ng’hami Industries Company Ltd.
Bashungwa amefikia maamuzi hayo baada ya kufika kiwandani hapo na kukagua bidhaa za kiwanda hicho ambayo ni unga wa viazi lishe na kugundua hazina nembo ya ubora ya TBS, ambayo changamoto hiyo imesababiswa na wafanyakazi wa shirika la TBS kwa kuwaomba fedha kwa ajiri ya kupewa nembo ya ubora pia kuchewesha kwa zaidi ya miezi saba bila kupewa majibu au nembo ya ubora.
Waziri Bashungwa baada ya kuona changamoto hiyo alimpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa TBS na DKt. Yusuph Ngenya na kumuelekeza kuwafukuza kazi wafanyakazi wake wanaokwenda kinyume na maagizo ambayo amekuwa akiyatoa mara kwa mara ya kutowachelewesha wafanyabiasha kwa sababu ambazo sio za msingi zinazosababisha bidhaa kutopewa nembo za ubora kwa wakati ambazo zinasababisha mazingira ya Rushwa na usumbufu kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Ntobi Rufunga ameeleza kuwa barua ya kuomba nembo ya ubora ilipelekwa TBS tangu mwezi 11, 2019 lakini mpaka sasa hajapewa majibu yoyote na baada ya kuchukuliwa kwa sampuli ya bidhaa hiyo wameombwa kutoa kiasi cha Tsh. 520,000/= ili wapewe nembo ya ubora ambayo ni kinyume na sheria na mashariti ya shirika hilo.
Aidha Bw. Ntobi amesema kuwa Kiwanda hicho mpaka sasa kinazalisha unga wa viazi lishe wa aina mbili ambao ni Unga wa kupika uji kwa ajiri ya matumizi ya rika zote pia Unga wa kutengeneza keki, mikate na andazi.
Social Plugin