Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mali za Benki na Uendeshaji CRDB Bw Beatus Segeja Pamoja na Jackton Koyi ambaye ni mteja wa Benki hiyo wakikata utepe kuashiria kuanza kwa huduma ya QR Code.
Moja ya Simu za Mteja akifanya majaribio ya huduma ya QR Code kwa ajili ya Kutoa maoni na kero zao kwa njia ya mtandao.
Mwandishi Wetu – Shinyanga
Ili kuishi katika Maneno na Kaulimbiu yake ‘CRDB Benki inayomsikiliza mteja’, Benki hiyo tawi la Shinyanga imezindua huduma mpya ya kidijitali ya kupokea maoni kutoka kwa wateja wake na wasio wateja kwa kutumia simu janja ujulikanao kama QR Code Scan.
Mfumo huo umezinduliwa Mapema leo Jumatatu ya Julai 27,2020 mjini Shinyanga katika tawi la benki hiyo likishuhudiwa na Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Bw Said Pamui, ambapo lengo ni kuhakikisha maoni ya mteja yanafika kwa wakati na kushughulikiwa mara moja kuliko ilivyokuwa awali walipokuwa wanapokea maoni kupita visanduku na kwa wahudumu wa benki hiyo.
Akizindua mfumo huo, Mkuu wa Kitengo cha Mali za Benki na Uendeshaji wake, Beatus Segeja amesema benki yao imekuwa ikiweka mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma na moja ya mikakati hiyo ni kuhakikisha wateja wanapata uhuru wa kutoa maoni popote walipo kulingana na huduma wanazozipata.
Segeja ameongeza kuwa benki yao inalenga kuongeza matumizi ya mfumo wa kidijsitali ili kutoa huduma kwa ufanisi na kwa uharaka zaidi, kwani mifumo hiyo ya kidijitali imeonyesha mafanikio makubwa ambapo asilimia 80 ya miamala katika benki hiyo mwaka 2019 imefanyika kwa njia ya kidijitali.
“Awali tulikuwa tunapokea maoni kupitia vituo vya huduma kwa wateja (Call centers), fomu maalum, wafanyakazi wetu na kwenye matawi, lakini sasa tumekuja na mfumo wa ukusanyaji maoni kidijitali kwa urahisi kupitia simu janja (QR code ) ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuwasikiliza wateja kwa sababu maoni ya wateja ni muhimu katika kuboresha huduma zetu,” amesema.
Amebainisha kuwa kutokana na kukuwa kwa teknolojia mahitaji ya wateja yamekuwa yakibadilika kila uchwao na kupelekea benki hiyo kutilia mkaozo utoaji wa huduma bora kwa njia ya kidijitali katika mpango mkakati wake wa biashara wa 2018-2022.
Naye Meneja wa Mambo ya ubora wa huduma, Bi Queen Odunga, amesema kuwa mfumo huo ni huru wa kukusanya maoni kutoka wateja wa benki hiyo na wasio wateja wanaopata huduma kwenye matawi na ATM maeno yote ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao kwani imekuwa sehemu ya kwenda na wakati.
“Tunafanyia kazi maoni kwa wakati na tunamrejea mteja kumshukuru kwa maoni yake na kumpa mrejesho wa kile alichokitoa, kila mteja anapojisikia kwamba amehudumiwa vizuri ama vibaya asisite kutoa maoni yake kwa sababu itatusaidia benki kuendelea kukua kwa pamoja na wateja,” amesema Bi Queen.
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Bw Said Pamui amesema kuwa benki hiyo imekuwa msitari wa Mbele katika kuboresha huduma zake ili kurahisisha hutoaji wa huduma kwa wateja wake
.
.
Mmoja wa wateja wa benki hiyo aliyehudhuria hafla ya uzinduzi wa mfumo huo, Grace Mng’ong’o ambaye ni Mkurugenzi wa Gven Wear, amesema huduma hiyo ni rafiki na huru kwa wateja kutoa maoni kwani hapo awali mfumo uliokuwepo haukuwa rafiki wateja wachache waliopata nafasi ya kuonana na wahudumu kueleza kero zao.
Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mali za Benki na Uendeshaji CRDB Bw Beatus Segeja pamoja na Baadhi ya wakuu wa idara toka makao makuu CRDB Bank.
Meneja wa CRDB Tawi la Shinyanga Bw Luther Mneney akizungumza kuwakaribisha wageni wote waliohudhuria hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa huduma ya QR Code.
Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Magharibi Bw Said Pamui Kulia akifuraha jambo na Meneja wa Tawi la Shinyanga Bw Luther Mneney kabla ya uzinduzi.
Meneja wa CRDB Kanda ya Magahribi Said Pamui akionyesha wateja wao huduma mpya inayoanza kufanya kazi katika tawi la Shinyanga ya kupokea maoni kwa njia ya Mtandaoa
Mkuu wa Kitengo cha Mali za Benki na Uendeshaji CRDB Bw Beatus Segeja akifurahia jambo baada ya kueleza umuhimu wa kutumia QR Code.
Katikati ni Meneja wa Mambo ya Ubora wa huduma CRDB Makao Makuu Bi Queen Odunga
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Makao Makuu na Kanda ya Magharibi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkuu wa Kitengo cha Mali za Benki na Uendeshaji CRDB Bw Beatus Segeja na Meneja wa Mambo ya Ubora wa huduma CRDB Makao Makuu Bi Queen Odunga katika picha ya pamoja
Meneja wa Mambo ya Ubora wa huduma CRDB Makao Makuu Bi Queen Odunga akieleza namna mfumo huo unavyofanya kazi.
Bw Jacton Koyi Mmoja wa wateja wa CRDB Bank tawi la Shinyanga akifanya majaribio ya kutumia mfumo wa QR Code utakaomwezesha kutoa maoni yake kwa njia ya kidijitali
Majaribio yakiendelea kwa wateja wa benki hiyo
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Bw. Said Pamui akifanya majaribio ya Mfumo wa QR Code
Mmoja wa Wateja wa benki hiyo akiendelea kupata huduma ya QR Code na kutoa Maoni yake
Wateja wakiendelea kupata elimu ya Namna ya kutumia Mfumo mpya
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Grace Mng’ong’o akifanya majaribio ya mfumo mpya wa utoaji maoni kwa njia ya Mtandao.
Baadhi ya wafanyakazi wa CRDB wakifanya maombi kwa dakika moja ikiwa ni Sehemu ya Maombolezo ya kifo cha Rais wa Awamu wa tatu Benjamini Mkapa alyefariki Julai 24 Mwaka huu Jijini Dar es salaam.
Tazama Picha zaidi hapa chini