Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TUNDU LISSU KUTUA TANZANIA KESHO...KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kesho Jumatatu Julai 27,2020 Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu atarejea nyumbani nchini Tanzania na kesho kutwa Julai 28,2020 atahudhuria shughuli za utoaji wa heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 26, 2020, na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho Tumaini Makene.

Amesema Tundu Lissu anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania Siku ya Jumatatu Julai 27,2020 majira ya saa saba na dakika 20 mchana ambapo atatua katika ardhi ya Tanzania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akisafiri na shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) kutokea Ubelgiji.

Aidha Makene amesema siku ya Jumanne Julai 28,2020 , Tundu Lissu atahudhuria shughuli ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu Hayati Benjamin William Mkapa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam na kwamba ratiba ya shughuli zingine zitatolewa.
SOMA ZAIDI <<HAPA>>
Via EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com