Picha: SWALA YA EID AL - ADHA YAFANYIKA UWANJA WA SABASABA SHINYANGA MJINI...SHEIKH BALISUSA ATAKA AMANI ITAWALE UCHAGUZI MKUU


Na Marco Maduhu - Shinyanga
Shekh Balilusa Khamisi wa mjini Shinyanga, amewataka viongozi wa vyama mbalimbali vya kisiasa hapa nchini pamoja na wanachama wao, kudumisha amani katika uchaguzi mkuu, utakaofanyika Oktoba mwaka huu wa kuchagua madiwani, wabunge na Rais.

Amebainisha hayo leo mara baada ya kumaliza kuongoza  swala ya Eid Al-Adha iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Shinyanga, kuwa matarajio ya viongozi wa dini ni kuona uchaguzi mkuu unakuwa tulivu na amani, na kusiwapo vurugu zozote zile za uvunjifu wa amani.

Sheikh Khamisi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamti ya amani mkoa wa Shinyanga, amesema viongozi wa siasa pamoja na wanachama wao, wanapaswa kutanguliza maslahi ya taifa mbele na siyo maslahi yao binafsi katika kipindi cha uchaguzi mkuu, na kutofanya vurugu ambazo zitavunja amani ya nchi na kuingia kwenye machafuko.

“Sisi kama viongozi wa dini tunawaomba sana viongozi wa kisiasa hapa nchi pamoja na wanachama wao, katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, watangulize maslahi ya taifa na siyo maslahi yao binafsi, ili kulinda amani ya nchi yetu na kutofanya vurugu zozote kwenye uchaguzi,” amesema Sheikh Khamisi.

Katika hatua nyingine amewataka wakuu wote wa shule binafsi kutowanyima wanafunzi muda wa kwenda kuswali masomo ya dini, kwa madai ya kufidishia muda uliopotea wakati wa kipindi cha likizo ya Corona, bali wawaruhusu ili wapate masomo hayo ya kiimani ambayo yatawajenga kimaadili.

Naye mjumbe wa baraza la Masheikh mjini Shinyanga Shekh Khalfan Ally, akitoa mawaidha amewataka waumini wa dini hiyo ya kiislam hasa vijana, kuzingatia miiko na sheria ya dini hiyo ili kutoporomoka kimaadili, pamoja na kuacha kuzaa watoto kabla ya kufunga ndoa na kutolelewa na majimama.

Aidha amesema baadhi ya vijana wa dini hiyo hawana maadili kabisa, ambapo wamekuwa wakifanya uzinzi na kuzaa watoto nje ya ndoa, kutovaa mavazi ya heshima, kunyoa mitindo ya nywele, pamoja na kupenda mteremko na kwenda kuoa wanawake wenye pesa bila hata ya kujali tabia zao wala umri bali wao wanajali pesa tu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Sheikh Balilusa Khamis akizungumza mara baada ya kumaliza kuongoza swala ya Eid Al-Adha  katika uwanja wa Sabasaba mjini Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog

Mjumbe wa Baraza la Mashekh mjini Shinyanga Shekh Khalfan Ally, akitoa mawaiza kwenye swala yaEid Al-Adha.

Shekh Balilusa Khamisi akiongoza maombi kwenye Swala ya Eid Al-Adha  kwenye uwanja wa uhuru mjini Shinyanga.

Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa kwenye swala yaEid Al-Adha  katika uwanja wa Sabasaba mjini Shinyanga.

Swala ikiendelea.

Swala ikiendelea.

Swala ikiendelea.



Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa kwenye  swala ya Eid Al-Adha.

Swala ikiendelea.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post