Na Ismaily Luhamba,Singida.
Waislam mkoani Singida leo wameungana na Waislam wenzao Duniani kutimiza Nguzo ya Tano ya Uislamu ya Sala ya Eid Al Adha ambapo swala hiyo mkoani Singida imefanyika kimkoa Wilayani Iramba kwenye Msikiti wa Tawqwa mjini Kiomboi.
Swala hiyo iliongozwa na Kadhi wa mkoa, Sheikh Ramadhani Kahoja.
Akisoma Khutuba, Mwandishi Maalum wa Mufti wa Tanzania Sheikh Harith Othman Nkusa atoa rai watu wapendanae hasa katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu ili nchi iweze kuvuka salama kama tulivyo weza kuvuka salama kwenye Janga la Corona.
"Pia Waumini na Wananchi tuwe watiifu kwa Viongozi wetu wa Serikali na wa dini zetu kwani kuwa Mtiifu sio utumwa ila ni kufuata sheria na kupenda Nchi yako. Sisi ndiyo tunaoweza kuijenga hii nchi na sisi pia tunaweza kuibomoa. Ndio maana nasisitiza utiifu kwa Waumini na wananchi kwa ujumla", alisema Sheikh Othman.
Naye, Katibu wa Bakwata mkoa wa Singida, Alhaji Burhani Mlau ametoa pole kwa Taifa kutokana na kifo cha Rais Mstaafu awamu ya tatu, Benjamin Mkapa aliyezikwa kijijini kwake, Lupaso wilayani Masasi mkoani Mtwara Jumatano hii.
"Kupitia swala hii ya Idd, napenda kusema tunakwenda kwenye Uchaguzi Mkuu wa nchi, sisi kama viongozi wa dini tuwe karibu sana na waumini wetu kwa kuwajenga kiimani na kuliombea Taifa letu ili liweze kuvuka salama kwenye uchaguzi huu" alisema Burhani.
Social Plugin