Vipando katika Banda la Rijk Zwaan Manyonyesho ya Kilimo Nanenane Mkoani Morogoro
Bwana Shamba wa Rijk Zwan Mkoani Morogoro Naiman Molel akiwa katika Kitalu nyumba (Green House) akielezea mazao yaliyopandwa ndani yake ikiwemo matiki matamu (Sweet melon) yanayozalishwa na kampuni hiyo
Bwana Shamba wa Rijk Zwan Mkoani Morogoro Naiman Molel akionyesha nyanya zinazolishwa na kampuni hiyo.
KAMPUNI ya uzalishaji wa Mbegu bora zenye kuleta tija kwa wakulima Rijk Zwaan yenye makao makuu yake Jijini Arusha imesema kuwa imejipanga kutoa elimu bora ya kilimo cha Kisasa kwa wakazi wa kanda ya mashariki watakaofika katika maonyesho ya Kilimo Maarufu kama nanenane Mkoani Morogoro.
Akizungumza katika eneo la Vipando la kampuni hiyo Mjini Morogoro Bwana Shamba wa Rijk Zwan Mkoani Morogoro Naiman Molel amesema kuwa wakulima wa kanda hiyo watapata fursa ya kuelimika juu ya mbegu bora za kilimo
Molel amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa takriban miaka mitano katika eneo hilo la nanenane na wamekuwa kwa kipindi chote hata baada ya maonyesho hayo.
Ameongeza kuwa hivi sasa watakuwa na mbegu mpya ya matikiti maji matamu ambayo yatakuwa yakipekee katika maonyesho hayo ya nane nane kanda ya mashariki
Sanjari na hayo ameeleza kuwa kampuni hiyo imendelea kutoa elimu kwa vikundi vya wakulima muda wote katika eneo la nanenane pasina malipo
Ameongeza kuwa hivi sasa wakulima pia wataelimishwa juu ya matumizi bora ya kitalu nyumba (green House) ambapo wataweza kuzalisha katika eneo dogo
Hata hivyo Bwana Shamba wa Rijk Zwan Mkoani Morogoro Naiman Molel ametoa wito kwa wakulima kufika katika banda hilo ili kuweza kuapata elimu zaidi
Maonyesho ya Kilimo 88 kanda ya Mashariki ya mwaka 2020 yana kauli mbiu maendeleo ya kilimo mifugo na uvuvi chagua viongozi bora huku yanahusisha mikoa ya Morogoro,Pwani,Tanga na Dar es salaam
Social Plugin