Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga ameshinda kwa kishindo uchaguzi wa kura za maoni
UWT mkoa wa Shinyanga kwa kupata kura 277 kati ya kura 335 zilizopigwa huku Kirumba Santiel Erick akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 155 na Mnzava Christina Christopher akishika nafasi ya tatu baada ya kupata kura 109.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika leo Alhamis Julai 23,2020 katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga,na kuhudhuriwa na Wajumbe wa mkutano mkuu UWT Mkoa wa Shinyanga, Msimamizi wa uchaguzi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewapongeza akina mama wote kwa kuingia kwenye kinyang'anyiro na kuwataka kuwa wamoja ili kupata ushindi katika uchaguzi mkuu.
"Kulikuwa na wagombea 42 lakini sisi tunahitaji watatu. naomba msiwe na kinyongo twende sasa tuwe timu moja tufanye kazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).Kwa sasa tubaki timu moja ya mkoa wa Shinyanga, akina mama tukiungana hatuwezi kupoteza kura hata moja",amesema Telack.
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuvunja makundi walivyokuwa nayo wakati wa mchakato wa uchaguzi huku akiwataka wale wenye malalamiko kuwasilisha malalamiko yao kwa maandishi ndani ya siku tatu.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Kura za maoni Ubunge Viti Maalum ambayeMkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack akitangaza matokeo ya uchaguzi. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Msimamizi wa Uchaguzi wa Kura za maoni Ubunge Viti Maalum ambayeMkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack akitangaza matokeo ya uchaguzi
Wajumbe wa mkutano wakiwa ukumbini.
Mmoja wa wagombea akiomba kura kwa wajumbe
Wagombea ubunge Viti maalum wakiwa ukumbini
Wagombea ubunge Viti maalum wakiwa ukumbini
Wagombea ubunge Viti maalum wakiwa ukumbini
Wajumbe wa mkutano wakiendelea na zoezi la upigaji kura
Wajumbe wa mkutano wakiendelea na zoezi la upigaji kura
Wajumbe wa mkutano wakiendelea na zoezi la upigaji kura
Wajumbe wakiwa ukumbini.
Wagombea wakiwa ukumbini.
Wagombea wakiwa ukumbini.
Wajumbe wakichukua karatasi za kupigia kura
Mjumbe akipiga kura
Zoezi la kupiga kura likiendelea.
Social Plugin