Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
Rais Magufuli ameahirisha sherehe za mashujaa zilizopaswa kufanyika Julai 25, 2020, Jijini Dodoma na kuwataka Watanzania kuitumia siku hiyo kuwakumbuka na kuwaombea mashujaa wote waliojitoa kwa ajili ya Tanzania.
Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 18, 2020, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, na kuongeza kuwa Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano.
Aidha Rais Magufuli pia amewataka Watanzania kuwaombea Mashujaa wote hata wale ambao wametoa mchango mkubwa katika ngazi mbalimbali, ikiwemo kwa mtu mmoja mmoja ama familia.
Social Plugin