WAJUMBE WA BODI YA MAJI SHUWASA WATEMBELEA CHANZO CHA UZALISHAJI MAJI ZIWA VICTORIA -IHELELE



Bodi ya Maji ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) pamoja na utawala wa mamlaka hiyo, wamefanya ziara ya kutembelea chanzo cha uzalishaji maji kutoka Ziwa Victoria kilichopo Ihelele wilayani Misungwi Jijini Mwanza, maji ambayo husambazwa mkoani Shinyanga na mikoa ya  jirani.


Ziara hiyo imefanyika leo Julai 24, 2020 ikiwa na lengo la kujionea namna maji yanavyozalishwa kutoka  Ziwa Victoria hadi kumfikia mwananchi na kuanza kuyatumia, ambapo chanzo cha uzalishaji maji hayo kinasimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama na Shinyanga (KASHWASA).

Akizungumza mara baada ya kumaliza kutembelea chanzo hicho cha maji, Mwenyekiti wa bodi hiyo ya maji kutoka SHUWASA, Mwamvua Jilumbi, amesema bodi yao ni mpya ndiyo maana wameona ni vyema kukifahamu chanzo cha maji kutoka Ziwa Victoria mahali kilipo na namna kinavyofanya kazi.

“Sisi ni bodi mpya ya maji kutoka Shuwasa, ambapo kila tunapokuwa tukikaa vikao wajumbe wamekuwa wakitaka kukijua chanzo cha uzalishaji maji kutoka Ziwa Victoria mahali kilipo na namna kinavyofanya uzalishaji huo wa kutoa maji ndani ya ziwa na kuyapeleka Shinyanga,”amesema Jilumbi.

“Ziara yetu hii imekuwa na mafanikio, ambapo tumeona wenyewe namna maji yanavyozalishwa kutoka ndani ya Ziwa Victoria na kuja SHUWASA na kumfikia mwananchi, na hata kama tukikaa kwenye vikao vyetu sasa hivi tutakuwa tunajua tunajadili nini,”ameongeza.

Pia ametoa pole kwa Rais John Magufuli pamoja na watanzania wote wakiwamo wana Shinyanga, kwa kuondokewa na Rais wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, ambaye ndiye muasisi kwa kupeleka maji hayo ya Ziwa Victoria mkoani humo, huku Waziri wa Maji kipindi hicho alikuwa  Waziri Mstaafu Edward Lowassa.

Naye Mkurugenzi wa mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) Flaviana Kifizi, amesema wamefanya ziara hiyo ili wajumbe wa bodi hiyo ya maji, wafahamu wapi huwa wananunua maji, na kisha kuyasambaza kwa wananchi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo ya maji KASHWASA John Zengo, alisema mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria ulianza kujengwa mwaka 2003 ukakamilika mwaka 2008 na mwaka 2009 ndipo ukaanza kusambaza maji safi na salama kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga 
ambapo mpaka sasa mradi huo umepanuka wanahudumia  pia Ngudu, Nzega hadi Tabora.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Fundi sanifu maabara ya maji kutoka KASHWASA Joseph Lugandya (mwenye koti jeupe) akitoa maelezo kwa wajumbe wa bodi ya maji ya SHUWASA, namna maji yanavyozalishwa kutoka ndani ya Ziwa Victoria.

Wajumbe wa bodi ya maji SHUWASA, wakiangalia mitambo ya kutoa maji ndani ya Ziwa Victoria na kuyapeleka kwenye eneo la kutibu maji hayo ili yawe salama kwa matumizi ya wananchi.

Wajumbe wa bodi ya maji Shuwasa, wakiendelea kuangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.

Wajumbe wa bodi ya maji SHUWASA, wakiendelea kuangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.

Wajumbe wa bodi ya maji SHUWASA, wakiendelea kuangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.

Wajumbe wa bodi ya maji SHUWASA, wakiendelea kuangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.

Wajumbe wa bodi ya maji SHUWASA, wakiendelea kuangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.
Wajumbe wa bodi ya maji SHUWASA, wakiendelea kuangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.

Wajumbe wa bodi ya maji SHUWASA, wakiendelea kuangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.

Muonekano wa eneo la kutibu maji yanayotoka ndani ya Ziwa Victoria kabla ya kwenda kutumiwa na wananchi.

Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi, akiwa na mjumbe wa bodi ya maji SHUWASA, wakiangalia namna maji yanavyotibiwa.

Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, kushoto, akiwa na mwenyekiti wa bodi ya maji SHUWASA  Mwamvua Jilubi, wakiangalia mabomba ya kupitisha maji yaliyotibiwa.

Wajumbe wa bodi ya maji SHUWASA, wakiwa kwenye Tenki la kuhifadhia maji mara baada ya kumaliza kutibiwa na tayari kutumiwa na wananchi.

Mkurugenzi wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi akipanda juu ya tenki la kuhifadhia maji.

Wafanyakazi wa SHUWASA na KASHWASA, wakiwa kwenye ziara ya wajumbe wa bodi ya maji SHUWASA, walipotembelea chanzo cha uzalishaji maji kutoka ndani ya Ziwa Victoria.

Wajumbe wa bodi ya maji SHUWASA, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutembelea chanzo cha uzalishaji maji kutoka ndani ya Ziwa Victoria- Ihelele Misungwi.

Wajumbe wa bodi ya maji SHUWASA, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutembelea chanzo cha uzalishaji maji kutoka ndani ya Ziwa Victoria- Ihelele Misungwi.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post