JERRY SILAA AONGOZA KURA ZA MAONI CCM JIMBO LA UKONGA

Jerry William Silaa 

 Na Andrew Chale

ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati kuu (CC)  ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa NEC, Jerry William Silaa amepata kura 206 huku mtia nia mwezake aliyemfuatia kwa karibu, Robert Masegese akipata kura 118 kwa kupitwa kura 88.


Katika zoezi hilo, jumla ya watia nia 147 walishiriki zoezi hilo, lililoanza mapema leo majira ya saa tatu asububi na kwenda hadi usiku huu.

Jerry Silaa ambaye aliwahi kuwa, Diwani wa Kata ya Gongolamboto na  pia Meya wa Ilala alitoa shukrani zake kwa kura alizopata.

Pia Jerry aliwahi kugombea nafasi ya Ubunge wa jimbo hilo la Ukonga, 2015.

Mwaka 2005  alianza kuwa Diwani katika Kata ya Ukong na baadae 2010 aligombea Udiwani Kata Gongolamboto na wakati huohuo aliweza kuwa Meya wa Ilala.

Jerry alisema 2015 aliamua kugombea Ubunge ili kuleta maendeleo zaidi katika Jimbo la Ukonga hata hivyo hakufanikiwa kupita na kutokukata tamaa na 2020 amemua kurejea tena kutimiza adhima yake hiyo.

Zoezi hilo lilisimamiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Idd Mkowa ambapo alisema zaidi ya wajumbe walioshiriki kupiga kura walikuwa zaidi ya 600.

"Kura 552 zilipigwa huku kura moja ikiharibika na kufanya kura halali kuwa 651."Alisema Mkowa.

Ambapo pia alimtaja Jerry Silaa, kupata kura 206.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post