TACAIDS YAKABIDHI MASANDUKU YA KUKUSANYIA FEDHA KUCHANGIA MFUKO WA KUDHIBITI UKIMWI SHINYANGA



Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko akimkabidhi masanduku 10 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Beda Chamatata kwa ajili ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuchangia Mfuko wa Kudhibiti UKIMWI nchini  leo Alhamis Julai 24,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko akimkabidhi masanduku 10 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Beda Chamatata kwa ajili ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuchangia Mfuko wa Kudhibiti UKIMWI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko akizungumza wakati wa akikabidhi masanduku 10 katika Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya wananchi kuchangia Mfuko wa Kudhibiti UKIMWI nchini. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko akihamasisha wananchi kuchangia Mfuko wa Kudhibiti UKIMWI. 
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Beda Chamatata akizungumza wakati akipokea masanduku 10 kwa ajili ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuchangia Mfuko wa Kudhibiti UKIMWI.
Mratibu wa Shughuli za Kudhibiti  UKIMWI Mkoa (RFP), Tedson Ngwale akifafanua kuhusu Masanduku ya kukusanyia fedha za mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI ( AIDS Trust Fund-ATF).
Muonekano wa moja ya Masanduku ya kukusanyia fedha za mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI ( AIDS Trust Fund-ATF).
Muonekano wa moja ya Masanduku ya kukusanyia fedha za mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI ( AIDS Trust Fund-ATF).
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imekabidhi masanduku 10 yatakayotumika kuchangia fedha katika mkoa wa Shinyanga ili kutunisha Mfuko wa Kudhibiti UKIMWI kwa ajili shughuli za kudhibiti UKIMWI nchini.

Masanduku hayo yamekabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko leo Alhamis Julai 24,2020 kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Beda Chamatata katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Dkt. Maboko alisema moja ya majukumu ya TACAIDS ni kutafuta fedha ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za UKIMWI hapa nchini ndiyo maana serikali iliona umuhimu wa kuanzisha mfuko wa Kuchangia Mfuko wa Kudhibiti UKIMWI kwa sababu fedha za wafadhili zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka.

"Serikali baada ya kuona fedha za wafadhili zinaendelea kupungua mwaka hadi mwaka ikaona ni vizuri kukawa na mfuko ambao utachangia na Watanzania wenyewe, serikali yenyewe na wananchi wenyewe sababu kubwa ikiwa ni kuziba mwanya au pengo linaloachwa na wafadhili katika mapambano dhidi ya UKIMWI nchini Tanzania",alisema Dkt. Maboko.

“Hii pesa mwisho wa siku inapokusanywa inakwenda kusaidia wananchi wenyewe. Haya maboksi 10 tunayakabidhi mkoa wa Shinyanga leo,tayari tulishakabidhi Geita,Simiyu,Kagera na yatakabidhiwa pia katika mkoa wa Mwanza",aliongeza. 

Aidha alibainisha kuwa kila mkoa utaamua wenyewe kuyaweka masanduku hayo katika maeneo yake ya kimkakati mfano kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa, wilaya, Mkurugenzi au popote penye mkusanyiko wa watu wengi na wananchi wanaweza kuchangia fedha kupitia namba ya simu 0684 90 90 90.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Beda Chamatata alieleza kufurahishwa kuhusu kuanzishwa kwa mfuko huo hali ambayo itawezesha Watanzania kujitegemea na kwamba Masanduku hayo yatagawiwa kwa Wakuu wa wilaya, halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga na jingine litabaki katika ofisi ya Mkuu wa mkoa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
أحدث أقدم