Mkurugenzi wa Takukuru Brigedia Jenerali John Mbung'o
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetekeleza maagizo ya Rais Dkt John Magufuli ya kuondoa madoa ya uwepo wa viashiria vya rushwa kwa baadhi ya watumishi wake baada ya kusimamisha watumishi tisa wa kitengo cha usimamizi wa miliki.

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi wa Takukuru Brigedia Jenerali John Mbung'o amesema uamuzi wa kuwasimamisha Jarudi Nyakongeza, Adam Mandia, Fortunatus Ngailo, Mohamed Kichewele, Nathaniel Otieno, Wilhelm Chuwa, Hamis Masoud, Mbwana Malumbo na Benedict Mabula ni ili kupisha uchunguzi dhidi yao.
Aidha, Brigedia Jenerali Mbung’o amesema ameunda tume huru kutoka nje ya Takukuru itakayochunguza value for money (thamani ya fedha) ya majengo saba ya taasisi hiyo yaliyojengwa wilaya za Chamwino, Mpwapwa, Ngorongoro, Manyoni, Masasi, Namtumbo na Ruangwa.
Katika hatua nyingine Mbung’o amesema amevunja kitengo cha usimamizi wa miliki Takukuru ili kiweze kusukwa upya.Uamuzi huo wa Mkurugenzi wa Takukuru unatokana na hatua ya Rais Dk. John Pombe Magufuli jana kutoridhishwa na gharama kubwa iliyotumika kujenga majengo yao hayo kwenye
Social Plugin