Viongozi wa TIP na Waandishi wa habari
Na Ellukagha Kyusa - Buchosa
Imeelezwa kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya ushawishi kwa jamii kufahamu haki za mtoto na pale wanapoona haki hizo zinavunjwa wana wajibu wa kuibua vitendo hivyo viovu na kuvifuatilia kuhakikisha watuhumiwa wanawajibishwa.
Hayo yamesemwa na Afisa ufuatiliaji na tathmini Mradi wa Boresha kutoka halmashauri ya Buchosa Bi.Amina Ally ambapo alisema viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kusaidia kupiga vitendo vya ukatili wa kingono kwa watoto.
"Viongozi wa dini wana wafuasi wengi kwenye nyumba zao za ibada hivyo wakitumiwa vizuri wanaweza kutoa ushawishi mzuri kwa jamii kufahamu haki za mtoto na pale wanapoona haki hizo zinavunjwa wao wana wajibu wa kuibua vitendo hivyo viovu na kuvifuatilia kuhakikisha watuhumiwa wanawajibishwa",alisema Amina.
Alisema Umoja wa Taasisi za Dini (TIP) inayojumuisha taasisi nne za kidini zikiwemo, Baraza wa Waislamu Tanzania ( BAKWATA), Umoja wa Makanisa ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Maaskofu (TEC) na ofisi ya Mufti Zanzibae (MoZ) unatekeleza miradi miwili ya kijamii katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema kwa lengo la kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI na ukatili wa kijinsia kwa watoto.
Afisa Ufuatiliaji na Tathimini wa Mradi wa Boresha, Amina Ally anasema miradi hiyo inalenga kutoa elimu kwa viongozi wa dini ili waweze kuielimisha jamii kuwa na tabia ya kupima virusi vya UKIMWI kwa hiari na pia kuepusha unyanyapaa kwa waathirikia wa UKIMWI.
Aliongeza kuwa mradi wa pili unalenga kutoa elimu kwa viongozi wa dini juu ya kupinga ukatili wa kingono kwa watoto na kwamba miradi hiyo ilisainiwa mwaka 2019 huku utekelezaji wake ukianza rasmi mwaka huu 2020.
Katika mradi wa Boresha TIP inatekeleza mradi mwingine wa kutoa elimu juu ya UKIMWI katika Halmashauri ya Buchosa na moja ya kazi ni kuwatumia viongozi wa dini kuhimiza waumini wao kupima Virusi vya UKIMWI na pia kutoa elimu ya kutokomeza unyanyapaa dhidi ya watu wenye maambukizi, kuhimiza matumizi ya dawa za kuongeza kinga za mwili.
Aidha khasim Hamis Gabo ambae Ni msimamizi wa mradi wa Boresha katika Halmashauri ya Buchosa amebainisha uwepo wa
changamoto mbalimbali kwenye ujazaji wa PF3.
Bi Gabo ametaja moja ya changamoto ya PF3 ni ujazaji mbaya wa fomu hiyo inayotokana na wananchi kukosa elimu ya kutosha wa namna ya kujaza, hali inayosababisha kupotea kwa ushahidi mara kesi inapofika Mahakamani.
Ameongeza kwa kusema kuwa, elimu zaidi inahitajika kwa jamii ili ifahamu umuhimu na kujaza vizuri fomu ya PF 3.