Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANAMKE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUWANYANYASA KINGONO WATOTO 7 WA KIKE


Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Irene James mwenye umri wa miaka 36 amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Tabora akituhumiwa kuwafanyia unyanyasaji wa kingono Watoto saba wa kike  jirani zake wenye umri kati ya miaka 4 hadi 7 kwa kuwaingizia vidole sehemu za siri.

Akisoma maelezo ya kosa jana Julai 30,2020 Wakili upande wa Jamhuri Gladness Senya ameieleza mahakama kwamba mtuhumiwa anadaiwa kutenda makosa hayo saba ya udhalilishaji wa kingono wa hali ya juu kinyume cha kifungu cha 138 C (1) (a)na kifungu kidogo cha 2(b) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019,Kitendo ambacho amekifanya kwa Watoto hao saba ambao majina yao yamehifadhiwa.

Mbele ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora John Mdoe Wakili huyo wa Jamhuri Gladness Senya alidai kuwa mtuhumiwa aliwatendea makosa hayo watoto hao saba wa majirani zake kwa nyakati tofauti majira ya mchana terehe zisizojulikana kati ya mwezi Januari hadi Julai mwaka huu huko katika Kata ya Kanyenye manispaa ya Tabora.

Hata hivyo mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora imemnyima dhamana mshitakiwa huyo kwa madai ya usalama wake na kwamba amepelekwa mahabusu mpaka pale kesi hiyo itakapotanjwa tena tarehe 13 mwezi Agust.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com