Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum (CCM) akionesha fomu ya kuwania ubunge wa jimbo la Solwa masaa mawili baada ya kuichukua.
Na Mwandishi wa Malunde 1 blog
Ahmed Salum ambaye anatetea kiti chake amechukua fomu ya kuomba kugombea ubunge Jimbo la Solwa leo Julai 14, 2020 saa 2 asubuhi na kuirejesha saa 4 asubuhi katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Akizungumza baada ya kurejesha fomu, Salum amesema anawashukuru viongozi wa chama hicho kwa kutengeneza mfumo mzuri wa kidemokrasia katika kupata wagombea ambao unatoa demokrasia ndani ya chama.
“Kikubwa tuchukue fomu tujaze tumtangulize Mungu, tusubiri mchakato ndani ya chama endapo jina langu likipendekezwa kama mgombea wa CCM ndipo nitazungumza zaidi,” amesema.
Ahmed Salum akisalimiana na baadhi ya wanawake waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania udiwani (Viti maalum) jimbo la Solwa.
Social Plugin