Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi. Jimbo hilo lilikuwa linaongozwa na Halima Mdee (Chadema).
“Kwa sasa itoshe tu kwamba nimechukua fomu,” amesema Askofu Gwajima muda mfupi baada ya kuchukua fomu.
Kwenye foleni hiyo, alikuwemo Abbas Tarimba, aliyekuwa kiongozi katika Timu ya Mpira ya Yanga na Diwani wa Kata ya Hananasifu ambaye anaomba ridhaa ya kugombea Jimbo la Kinondoni.
Mbunge anayemaliza muda wake kwenye jimbo hilo ni, Maulid Mtulia wa CCM.
Social Plugin