BALOZI WA TANZANIA NCHINI MISRI AKARIBISHA KIWANDA CHA NYAYA CHA CAIRO KUWEKEZA NCHINI
Friday, July 24, 2020
Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Meja Generali (Mst.) Anselm Shigongo Bahati akifanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya Giza Power kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya pande mbili. Kampuni hiyo inamiliki kiwanda kikubwa cha kutengeneza nyaya za umeme kwa matumizi mbalimbali. Kadhalika, Mhe. Balozi Bahati alitembelea kiwanda hicho na kujionea uwezo wa uzalishaji wa kiwanda hicho na kujadili na uongozi wa kiwanda hicho kuhusu kuja kuwekeza Tanzania. Kiwanda cha Giza Power kinafanya biashara ya nyaya za umeme na nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika.
Mhe. Balozi Bahati akipata maelezo kutoka kwa mtaalam alipokitembelea kiwanda kikubwa cha kutengeneza nyaya za umeme kwa matumizi mbalimbali. Kwenye ziara hiyo Mhe. Balozi Bahati alijionea uwezo wa uzalishaji wa kiwanda hicho. Kiwanda cha Giza Power kinafanya biashara ya nyaya za umeme na nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin