Wananchi wa Kijiji cha Weigita wakiwa kwenye barabara ambayo imekuwa kero kwao kwa miaka mingi bila matengenezo,na imekuwa ikitumika kama mradi kwa wanasiasa wakati wa kampeni za ubunge na Udiwani wakidai wakichaguliwa wataitengeneza lakini wakishapata uongozi hakuna utekelezaji.
Na Dinna Maningo,Tarime
Ubovu wa Barabara katika kijiji cha Weigita Kata ya Kibasuka wilayani Tarime mkoani Mara umekuwa ukitumika kama mradi kwa wanasiasa wanaogombea nafasi ya Ubunge na Udiwani kwa kuahidi kuitengeneza iwapo wakichaguliwa lakini imekuwa ni ndoto ujenzi kutekelezwa.
Inaelezwa kuwa wakati wa kampeni wanasiasa wamekuwa wakiwaahidi wananchi wa kijiji hicho kuwa endapo wakiwachagua watahakikisha barabara hiyo inatengenezwa lakini pindi wapatapo nafasi za uongozi huitelekeza barabara hiyo.
Kutokana na ahadi hiyo ya uongo iliyodumu kwa zaidi ya miaka 30 kutoka kwa Wabunge na Madiwani wanaopata nafasi za uongozi wananchi wa Kijiji cha Weigita wameiomba Serikali kuwatengenezea barabara yenye urefu wa km 2 ambayo imewakwamisha kutekeleza shughuli za kijamii huku wagonjwa wakibebwa kwenye machela kupelekwa kituo cha afya Nyarwana.

Wakizungumza na Malunde 1 blog,wananchi hao walisema kuwa barabara hiyo imekuwa kero kwa muda mrefu ambapo wagonjwa na wajawazito hulazimika kubebwa kwenye machela kuwafikisha kwenye huduma za afya.
Mmoja wa wananchi hao, Chacha Ryoba alisema nyakati za uchaguzi wagombea wanapofika kijijini hapo wamekuwa wakiahidi kuhakikisha inatengenezwa lakini wanapochaguliwa huishia mitini bila kutekeleza ahadi yao ya barabara.
Steven Nyaboncho alisema kuwa tangu azaliwe mwaka 1969 shida kubwa iliyopo ni barabara ambayo imekuwa ni kero kwa wananchi hivyo wanamuomba Rais Magufuli kuingilia kati ili kuhakikisha barabara inatengenezwa.
"Hivi Karibuni alikuja Naibu Waziri wa Tamisemi Mwita Waitara ilibidi magari yapaki barabara kuu wakatembea kwa miguu akachoka ikabidi akae pikipiki akatuahidi barabara itatengenezwa haraka iwezekanavyo lakini mpaka sasa bado na barabara hii imekuwa ni mradi wa wanasiasa kila anayefika anasema mkinipa kura nitawatengenezea barabara akichaguliwa anaishia mitini bila kutekeleza ahadi",anasema Nyaboncho.
Mnanka Nyaswi alisema kuwa nyakati za mitihani ya Taifa wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule ya msingi Nyambeche na Weigita hulazimika kujitwisha vichwani mitihani kuipeleka shule kwa kuwa gari haziwezi kupita kutokana na ubovu wa barabara.
"Barabara ni mbovu gari haiwezi kupita hata pikipiki zinapita kwa shida ikifika wakati wa mitihani wazazi wanaibeba vichwani kupeleka shuleni,wagonjwa wakizidiwa tunawabeba kwenye machela kuwapeleka kituo cha afya Nyarwana umbali wa kilomita 8 tunateseka sana",alisema Nyamswi.
Shukrani Hussein aliongeza "Wakati nikiwa darasa la tano mwaka 2010 yaliletwa madawati yakashushiwa barabara kuu ikashindikana kupelekwa shuleni ikabidi wanafunzi tubebe mengine yalifika yamevunjika hii barabara inakwamisha mambo mengi".
Manchori Bega mwendesha pikipiki alisema kuwa ubovu wa barabara unawalazimu kupandisha gharama za usafiri "Mvua ikinyesha tunakwama sehemu ambayo ungetumia usafiri shilingi 1000 abiria analazimika kulipa 3000 na pikipiki zinawahi kuharibika", alisema Bega.
Nyagonchera Chacha alisema kuwa baadhi ya wagonjwa hupoteza maisha kwa kushindwa kutembea kwa miguu ili kufika kwa wakati hospitali kupata huduma huku wajawazito wengine wakijifungulia njiani na nyumbani kwasababu ya umbali.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyanchage Matiko Wambura alisema kuwa licha ya kata hiyo kuongozwa na upinzani Chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema ngazi ya Udiwani na Ubunge na halmashauri ya wilaya ya Tarime kuongozwa na CHADEMA hakuna utekelezaji kuhakikisha barabara inatengenezwa.
"Huko Nyuma tuliichagua CCM na wakati wa kampeni walisema wakichaguliwa watatutengenezea barabara lakini walipochaguliwa hawakutengeneza ikafika wakati wananchi wakachukia na kugeukia upande wa upinzani wakamchagua Diwani wa upinzani na Mbunge ambao waliwahakikishia wananchi kutengeneza barabara lakini nao ni walewale ambapo halmashauri hiyo imeongozwa na Chadema lakini nao wameshindwa kutupigania ,kwa kuwa Rais wetu ni msikivu tunamuomba atutengenezee barabara maana hawa wapinzani nao wametudanganya na kwa sasa hatutaki tena upinzani tutaichagua CCM ",alisema Wambura.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Weigita Magoko Msabi alisema kuwa tangu 1966 hawajawahi kutengenezewa hiyo barabara ambayo imeleta shida kwa wasafiri na kwamba kutokana na ubovu wa barabara Zahanati iliyojengwa kwa nguvu za wananchi imeshindwa kutengamaa ili kutoa huduma kutokana na ubovu wa barabara ambao umesababisha vifaa vya ujenzi visifike kwa wakati
"Tumepata fedha shilingi milioni 12 ili kukamilisha ujenzi lakini tumeshindwa vifaa vitasafirishwaje barabara ni mbovu Simenti,mchanga,mawe yatapitishwaje gari haliwezi kupita,kuna wakati wazazi wanalazimika kuwabeba wanafunzi mgongoni kuwapeleka shule has a wa chekechea na darasa la kwanza kwenda hospitali nako ni shida",alisema Msabi.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa Kijiji cha Weigita kina kaya zipatazo 1,500 na Wakazi 3,500 na kwamba hitaji kubwa la wananchi ni Barabara,Zahanati na Maji hivyo anaiomba Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kuwatengenezea barabara kama inavyotekeleza huduma za kijamii katika maeneo mbalimbali ya hapa nchini.
Meneja wa Wakala wa Barabara za mjini na Vijijini halimashauri ya wilaya ya Tarime(TARURA) TARURA Hatibu Nunu alipohojiwa kufahamu ni lini barabara hiyo itajengwa ili kuwaondolea adha wananchi wa kijiji cha Weigita alisema kuwa tayari barabara hiyo imetengewa fedha katika mwaka huu na ujenzi utaanza hivi karibuni japo hakutaja kiasi cha fedha kilichotengwa wala muda wa kuanza kwa ujenzi huo wa barabara.
Wananchi wa Kijiji cha Weigita wakiwa kwenye barabara ambayo imekuwa kero kwao kwa miaka mingi bila matengenezo,na imekuwa ikitumika kama mradi kwa wanasiasa wakati wa kampeni za ubunge na Udiwani wakidai wakichaguliwa wataitengeneza lakini wakishapata uongozi hakuna utekelezaji.
Zahanati ya Kijiji cha Weigita iliyojengwa kwa nguvu za wananchi tangu 2014 lakini haijakamilika kutokana na ubovu wa barabara uliosababisha gari kushindwa kupita kupeleka vifaa vya ujenzi
Social Plugin