Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje ya nchi wa Tanzania,na kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Benard Membe,amerejesha kadi ya uanachama wa Chama hicho.
Membe amerejesha kadi hiyo leo Jumatatu tarehe 6 Julai 2020 nyumbani kwake Rondo mkoani Lindi.
“Leo saa 6 na nusu mchana mimi na mke wangu nikisindikizwa na mamia ya wananchi wa Rondo, tumerejesha kadi zetu za CCM kwa wenyewe. Nimemwandikia KM (katibu mkuu) wa CCM kuhusu tukio hilo na kukishukuru chama kwa mema yote kilichonitendea. Nawatakia kila la heri viongozi na wanachama wote,” ameandika Membe kupitia ukurasa wake wa Twitter
Tarehe 28 Februari 2020, Kamati Kuu ya CCM ilitangaza kumfukuzwa uanachama Membe kwa madai amekuwa akikiuka taratibu na miongozo ya chama hicho
Social Plugin