Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameweka wazi kuwa kesho Julai 16, 2020 watambambulisha rasmi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Bernard Membe kuwa mwanachama rasmi wa chama hicho.
Zitto ameweka wazi hayo kwenye ujumbe alituma kwenye ukurasa wake wa twitter akiwa ameweka picha ya Membe hukua akiwa ameshikiria kitabu cha ACT-Wazalendo.
Amesema, Membe atatambulishwa kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa mlimani City mbele ya wanachama wa chama hicho.
Kwa muda mrefu sasa Bernard Membe amekuwa akihusishwa na kuhamia kwenye chama cha ACT wazalendo baada ya kufukuzwa CCM kwa madai ya kukiuka baadhi ya taratibu za chama hicho.
Social Plugin