Bunge la Somalia limepiga kura ya kumwondoa kwenye wadhifa wake Waziri Mkuu Hassan Ali Khayre, ambaye ameendelea kusolewa kutokana na jinsi anavyoishughulikia hali ya usalama nchini humo.
Wabunge wamepiga kura ya kumuachisha kazi Hassan Ali Khayre kwa kura 170 na wabunge wanane wamepiga kura ya hapana, ametangaza spika wa bunge la Somalia.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed amesema katika taarifa kwamba anakubali uamuzi wa bunge kumtimua waziri mkuu.
"Hivi karibuni atamteua waziri mkuu mpya," imesema sema taarifa hiyo