Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHADEMA YAFUNGUA PAZIA KWA WAGOMBEA WA URAIS, UWAKILISHI NA UDIWANI ZANZIBAR


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema, fomu za kuwania urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 zitaanza kutolewa kuanzia Julai 4 hadi 19, 2020.


Hayo yamesemwa leo Jumatano tarehe 1 Julai 2020 na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salumu Mwalimu alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa kumpata mgombea urais, ubunge na uwakilishi.


Amesema, mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu kwa mwanachama wa chama hicho anayetaka kugombea Urais wa Zanzibar utahitimishwa saa 10:00 jioni ya tarehe 19 Juni 2020.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com