Mtaalam wa Kodi na Maendeleo ambaye pia ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Andrew Chale (kushoto) akikabidhi fomu ya kutia nia kiti cha Ubunge CCM-Mbagala wakati wa kurejesha.
**
Mtalaamu wa Kodi na Maendeleo ambaye pia ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM , Andrew Chale, amechukua na kurejesha fomu ya kutia nia kiti cha Ubunge CCM-Mbagala.
Andrew Chale amekuwa ni miongoni mwa Vijana walioguswa na utekelezaji wa CCM kuruhusu Demokrasia pana kwa kila mwenye nia kujitokeza kuongoza.
"Nimekuwa mdau mkubwa wa Maendeleo kwa kusaidia masuala ya mbalimbali ya kijamii Vikundi vya Vijana na makundi maalum ndani na nje ya Wilaya yangu.
"Kwa sasa shauku yangu ni kuongoza wananchi ndani ya Jimbo hivyo nimetimiza haki yangu ya kuchukua na kurejesha fomu na kwa sasa nasubiria hatua ndani ya chama" Alisema Andrew Chale.
Aidha, Alieleza kuwa, kwa sasa Vijana wanataka kuona safari ya Mbagala mpya yenye maendeleo na miondombinu ya kisasa inatimia.
Social Plugin