MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati akifungua
kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi wilaya ya Muheza kulia ni
Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Flora Kessy
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati akifungua
kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi wilaya ya Muheza kulia ni
Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Flora Kessy
Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Flora Kessy akizungumza wakati wa kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wilayani Muheza Julias Mgeni akizungumza wakati wa kikao hicho
Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wilayani Muheza Julias Mgeni akizungumza wakati wa kikao hicho
MRATIBU wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Mkoa wa Tanga Dkt Rehema Maggid akizungumza katrika kikao hicho |
mmoja wa washiriki kwenye kikao hicho akichangia jambo
sehemu ya wajumbe kwenye kikao hicho
MKUU
wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mhandisi Mwanasha Tumbo amewataka
viongozi wa dini wa taasisi za serikali na binafsi washirikiana
kuwahamasisha jamii na wananchi wakijitokezea kwenye unywaji wa dawa za
kutokomeza ugonjwa minyoo ya tumbo na usubi.
Mhandisi Mwanasha
aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya
Msingi wilaya ya Muheza ambapo alisema kwamba kumekuwa na fikra potofu
kwamba dawa hizo zinazuia uzazi au kusababisha kansa lengo kutokomeza
ugonjwa wa m inyoo na tumbu na usubi.
Alisema kwa Sasa hawatoi
dawa za kuzuia na kujikinga na matende kwa sababu wameweza kuudhibiti
kwa asilimia kubwa ugonjwa huo huku akieleza mwengine uliokuwepo na sasa
umekwisha ni mabusha kutokana na kufanya operesheni nyingi na umekwisha
,
Alitoa
wito kwa jamii kama wapo wengine wenye matatizo hayo wajitokeza na
kupatiwa matibabu na yaweze kwisha kabisa kwa jamii na hatimaye kuweza
kuumaliza kabisa kwenye maeneo hayo.
Alisema kipindi cha nyumba
walikuwa wanasumbuliwa na ugonjwa wa matendo na usubi mara nyingi
hawayapewi kipambele wanakuwa hawafuatilii tiba matokeo yake wakawa
wanaambukizana.
“Usubri upo hasa kandokandoi ya mito mtu anapata
ugonjwa wa macho anaona ni ugonjwa wa kawaida lakini hivi sasa
wamehakikisha wenye matende tunatoa kinga tiba kinga kama mtu anapata
basi Kuhakikisha wadudu hao wanakufa”Alisema
“Lakini takribani
muda mrefu wananchi wa muheza wamekuwa wakipewa dawa ya matende na
wilaya ya Muheza vipimo vimefanyika na kuonekana ugonjwa huo umekwisha
na jitihada hizohizo tunazielekeza kwenye usubi “Alisema DC Mhandisi
Mwanasha
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba hamasa hiyo kwa
wananchi sasa ni kuhakikisha wanajitokeza waliokuwa na madhara na
wasiokuwa nayo ili kuweza kupata kinga kwa sasa wamebakia asilimia 2.
Hata
hivyo alisema kwa upande wa wanafunzi wana sumbuliwa na minyooo
wameweka mikakati wanafunzi wote wahakikisha wanakunywa dawa za kuzuia
minyoo ili kuweza kudhibiti.
“Lengo la Serikali chini ya Rais
Dkt John Magufuli ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya njema waweze
kuendelea na shughuli za kiuchumi na kutekeleza kwa vitendo lakini pia
na wanafunzi kusoma kwa bidii”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Awali
akizungumza Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wilayani
Muheza Julias Mgeni alisema kwamba wilaya hiyo walianza kutokumeza
magonjwa manne ambayo ni kichocho, usubi, mabusha na matende, minyoo ya
tumbo.
Alisema kwa sasa kiwango cha maambukizi ya mabusha na
matende kipo chini ya asilimia mbili hivyo haewaendelei tena kutoa dawa
bali wanatoa elimu kwa walioathirika nalo ikiwemo upasuaji mabusha,
matende wanatoa elimu.