Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Gaspar Kileo (kulia).
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Gaspar Kileo maarufu 'GAKI' amechukua fomu ya kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Gaspar Kileo amechukua fomu leo Jumanne Julai 14,2020 katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ambapo Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu alikuwa anatoa fomu hizo kwa wanachama wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Gaspar Kileo amesema atazungumzia vipaumbele vyake mara baada ya chama chake kumpitisha kuwa mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Gaspar Kileo akiwa ameshikilia fomu ya kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu,kulia ni mtoto wa Gaspar, Kileo Gladness

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Gaspar Kileo akiwa ameshikilia fomu ya kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin