Mbunge wa Arusha Mjini anayemaliza muda wake, Godbless Lema amesema sheria ingeruhusu, angetaka wagombea wote wa CCM Arusha ashindane nao.
“Nime sikia sikia majina ya wagombea Ubunge Arusha Mjini kupitia ccm.Kama sheria ingeruhusu wote 30 kushindana nami na picha zao wote kutokea kwenye karatasi ya kura dhidi yangu,bado wangeimba wimbo walio imba 2010/2015.Twendeni mpaka mwanzo wa bahari,wepesi sana hawa.” ameandika Lema kwenye ukurasa wake wa twitter.
Leo, CCM imefungua pazia kwa wanachama wake kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hiyo, zoezi hilo linatarajiwa kusitishwa tarehe 17 Julai 2020.
Social Plugin