Baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanza zoezi la Utoaji wa Fomu za kugombea nafasi za Ubunge, na Udiwani katika Wilaya ya Kahama yenye Majimbo Matatu ya Msalala,Ushetu na Kahama Mjini mwitikio wa wagombea wanawake umekuwa mkubwa ikilinganishwa na Uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo mpaka sasa katika majimbo yote jumla ya wagombea wanawake 9 wamejitokeza kugombea nafsi hizo.
Bi Grace Rukanda, ambaye ni Mhasibu Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Kahama(KUWASA) leo Julai 15,2020 amechukua fomu ya kuomba Ridhaa ya kuchaguliwa kugombea Ubunge katika Jimbo La Kahama Mjini kupitia Tiketi ya (CCM) ambapo mpaka sasa linawagombea saba Wanawake.#
Social Plugin