Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT. MAYROSE MAJINGE ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHADEMA


Leo Julai 7, 2020, mwanachama wa CHADEMA  Dkt Mayrose Majinge, amejitokeza kuchukua fomu ya kuomba uteuzi wa kugombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.


Dk. Majinge amekabidhiwa fomu hiyo  na Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema Reginald Munisi, katika Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni, jijini Dar es Salaam. 


Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo , Dk. Majinge  ametaja  mambo kadhaa ambayo atayafanyia kazi endapo atachaguliwa na Chadema kugombea nafasi hiyo na kisha kupata ridhaa ya wananchi kuwa rais wa Tanzania.

Dk. Majinge amesema, endapo atapata ridhaa hiyo, atajenga mfumo imara na madhubuti  wa uongozi wa taifa, kwa ajili ya maslahi ya kizazi cha sasa na vijavyo.

Amesema ahadi yake kwa Watanzania ni kuwezesha upatikanaji wa katiba ya wananchi na tume huru ya uchaguzi


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com