Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PATROBAS KATAMBI AREJESHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI...ASEMA "KUPATA AU KUKOSA UBUNGE NI MIPANGO YA MUNGU"



Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi  akimkabidhi Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu Fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini  leo Ijumaa Julai 17,2020 majira ya saa nne asubuhi katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akiwa katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini baada ya kurudisha Fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini  leo Ijumaa Julai 17,2020 majira ya saa nne asubuhi.
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini baada ya kurudisha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini  leo Ijumaa Julai 17,2020 majira ya saa nne asubuhi.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amerejesha Fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.

Katambi amerudisha fomu hiyo leo Ijumaa Julai 17,2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu.

Akizungumza baada ya kurejesha fomu, Katambi ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumteua kuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma nafasi ambayo ameitumikia kwa kipindi cha miaka miwili tangu mwaka 2018 hadi leo Julai 17,2020 Rais Magufuli alipomteu Josephat Paulo Maganga kuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma.

“Namshukuru sana Rais Magufuli kwa kuniamini na kuniteua kuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma nafasi ambayo nimeitumikia kwa muda wa miaka miwili na matokeo makubwa mmeyaona, Dodoma tumepiga hatua kubwa kimaendeleo”,amesema Katambi.

“Hodi Shinyanga!,baada ya kufanya mambo makubwa Dodoma nimeona nirudi kwetu Shinyanga kuomba kugombea Ubunge kupitia CCM. Muda umefika sasa mimi kuwatumikia Wana Shinyanga. Nimejitoa sadaka kuacha U- DC ili nije niwatumikie wananchi wa Shinyanga, kuleta maendeleo kwa wana Shinyanga.

“Kupata Ubunge au kukosa ubunge ni mipango ya Mungu. Kama kura zitapungua kuniwezesha kugombea ubunge CCM basi nitarudi kufanya majukumu mengine ikiwemo yangu ya Uanasheria”,ameongeza Katambi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com