Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Myika, amesema hatagombea ubunge, katika jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam
Mnyika ambaye amekuwa mbunge wa Kibamba ambayo ilikuwa sehemu ya jimbo la Ubungo, kwa miaka 10 mfululizo, amesema amechukua hatua hiyo ili apate muda wa kutosha kutumikia nafasi yake ya sasa ya Katibu Mkuu CHADEMA.
"Haya nilisema kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu 2019, Nyerere aliwahi kuachia Uwaziri Mkuu akabaki kuimarisha TANU, nami sitagombea ubunge 2020, nitumikie ipasavyo Ukatibu Mkuu CHADEMA tushinde chaguzi." - ameandika John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mnyika alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa chama hicho Desemba mwaka 2019 akichukua nafasi ya Dk. Vicent Mashinji ambaye jina lake halikupendekezwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho .
Katika mkutano wa kura za maoni uliyofanyika jana Jumanne, tarehe 14 Juni 2020, Ernest Mgawe, mwenyekiti wa Chadema katika jimbo la Kibamba, alitangazwa mshindi. Mgawe alipata kura 30, kati ya 71 zilizopigwa.
Social Plugin