Saed Kubenea.
Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA Saed Kubenea, amesema kuwa maamuzi ya yeye kujiunga rasmi na chama cha ACT Wazalendo yalikuwa ni magumu, kwa kuwa hicho ndiyo chama chake cha pili kujiunga tangu aanze siasa na kudai kuwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam upinzani una nguvu kubwa.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 18, 2020, mara baada ya kujiunga rasmi na chama cha ACT Wazalendo, na kupokelewa na kukabidhiwa kadi ya uanachama na Mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
"Kwa kweli maamuzi haya yalikuwa ni magumu sana kwa sababu katika maisha yangu, hiki ndiyo chama cha pili kujiunga lakini nilifika mahali nikasema, kama Maalim Seif alinzisha CUF kwa jasho na damu akaondoka, baada ya kutoridhika na hali iliyokuwa ikiendelea sembuse mimi, nikajifunza kwamba ni lazima safari hii ya mabadiliko iendelee", amesema Kubenea.