Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 kwa tiketi ya CHADEMA.
Nyalandu amekabidhiwa fomu hiyo leo Jumatano tarehe 8 Julai 2020 na Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema Reginald Munisi katika Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Nyalandu amesema atarejesha umoja wa kitaifa na kuondoa tofauti za kisiasa.
“Jambo la kwanza ni kuhakikisha tunarejesha umoja wa kitaifa. Matumaini ya Watanzania ya udugu, upendano na ushirikiano, penye lawama tupeleke upendo.
“Wakati naondoka CCM nilisema, ili nchi iwe sawaswa ni lazima serikali, mahakama na bunge viwe huru. Haya mafiga matatu yanatakiwa yajitegemee na yajiendeshe pamoja,” amesema Nyalandu.
Social Plugin