Angalia Picha : RAIS MAGUFULI AKIWA NA WASANII MBALIMBALI IKULU CHAMWINO DODOMA...DIAMOND, ALIKIBA, HARMONIZE...


Na Alex Sonna,Dodoma
WASANII wa mziki wa Bongo fleva wamempagawisha Rais John Magufuli katika hafla ya chakula cha mchana na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) iliyofanyika Ikulu ya Chamwino.

Katika hafla hiyo, wasanii mbalimbali akiwemo Alikiba, Daimond Platnumz, Hamonize, Nandy, Zuchu, MwanaFA, Lavalava, kundi la Magufuli Gang likiongozwa na Shetta, Dogo Janja, Mrisho Mpoto, Bob Haiza,Rayvanny, Mbosso,Marioo, kundi la TOT na wasanii wengine, ambapo walipata fursa ya kutumbuiza na kukonga nyoyo za wajumbe wa mkutano huo.

Akizungumza namna alivyofurahishwa na mziki wao, Rais Magufuli amesema yeye ni shabiki sana wa nyimbo na huwa anafurahi sana.

“Nawashukuru sana wasanii kweli nimejisikia raha, unapomuona Alikiba amekaa pamoja na Daimond wamekaa pamoja unaiona nguvu ya CCM, leo unapomuona Harmonize aliyemkimbia Daimond anamsifia hadharani huu ndo utanzania ninao utaka, nawashukuru sana wasanii, asanteni sana kwa kuunga mkono Chama cha Mapinduzi,”amesema.

Amewataka waendelee kuitangaza Tanzania wasikate tamaa na kuwahakikishia siku zijazo mambo yatakuwa vizuri.

“Huwa nafurahi na nafuatilia kweli sijui nyimbo za Nandy za nani, endeleeni kuitangaza Tanzania, msikate tamaa tupo pamoja na nyinyi, endeleeni kukinadi Chama cha Mapinduzi, nataka kuwahakikishia siku zinazokuja mambo yatakuwa mazuri zaidi, nawashukuru mameneja wenu wote nawashukuru na waigizaji na wanamichezo wote kwa kazi kubwa ya kutangaza nchi yetu,”amesema.

Ameongeza “Kitendo mlichoonesha leo mkaoneshe hivyo hivyo, mapatano mliyofanya leo yakapate na nguvu ya Mwenyezi Mungu, ninyi ni vijana mmeanza vizuri nendeni hivyo na Mungu atawajalia zaidi.”

Tazama hapa chini Matukio katika picha ,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na wasanii waliofika pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho kutembelea Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Julai 12, 2020


 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post