Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Julius Masele (kulia).
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (2010 - 2020), Stephen Julius Masele amechukua fomu ya kuomba kugombea tena Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Stephen Julius Masele amechukua fomu leo Jumanne Julai 14,2020 katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ambapo Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Mashema alikuwa anatoa fomu hizo kwa wanachama wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Masele amesema sababu kubwa ya kuomba ridhaa ya wanachama wa CCM kumptisha kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini ni kukamilisha na kuendeleza kazi za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambazo amezifanya katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo.