Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWENYEKITI WA BARAZA LA VIJANA CHADEMA AUAWA KWA KUCHOMWA MSHALE


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto, amesema kuwa tayari jeshi hilo limemkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Mwenyekiti wa BAWACHA Kata ya Palanga Asia Said, aliyeuawa baada ya kuchomwa mshale usiku wa kuamkia leo wakati akiandaa chakula cha jioni yeye na mume wake.

Kamanda Muroto ametoa kauli hiyo hii leo Julai 23, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kusema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni mume wa marehemu anayejulikana kwa jina la Hassan Masale, kuwa na ugomvi na mtuhumiwa Haruna Ally, baada ya kuingiza mifugo kwenye shamba la Alizeti la mtuhumiwa wa mauaji ya mkewe.

"Tukio limetokea jana majira ya saa 2 usiku na alifariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Kondoa, na Mshale uliotumika umekamatwa na mtuhumiwa amekamatwa na amekiri kufanya tukio hilo", amesema Kamanda Muroto.

Kamanda Muroto ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo alifanya tukio hilo kwa lengo la kulipiza kisasi na ndipo alipomvizia mume wa marehemu wakati akiwa nje ili kumchoma mshale na kisha mshale huo kumpata mwanamke badala ya mwanaume.
Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com