Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje nchini Tanzania amekubali ombi la wanachama wa ACT-Wazalendo la kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020.
Membe ametoa kauli hiyo leo Ijumaa tarehe 17 Julai 2020 ikiwa ni siku moja kupita tangu alipopokelewa rasmi ndani ya ACT-Wazalendo jana Alhamisi katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
Mwanasiasa huyo amejiunga na chama hicho cha upinzani baada ya kufukuzwa ndani ya chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) alichokulia kwa kile kilichoelezwa hakuwa na mienendo inayoridhisha tangu mwaka 2014.
Jana niliombwa na leo nimekubali rasmi kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo. Huu ni wakati muafaka kwangu wa kushiriki katika mazungumzo na vyama vingine kama Chadema ili tusimamishe "KISIKI CHA MPINGO" kimoja!— Bernard K. Membe (@BenMembe) July 17, 2020
Social Plugin