Waziri wa Madini Doto Biteko akijipaka kitakasa mikono baada ya kupimwa joto kwenye mgodi wa Williamson Diamond Limited alipokuwa kwenye ziara yake Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjla akipimwa joto kabla hajaingia kwenye ukumbi wa mkutano katika mgodi wa Williamson Diamond Limited nyuma yake ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula.
Waziri wa Madini Doto Biteko akifafanua jambo kwenye kikao katika mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga |
Baadhi ya washiriki walioshiriki kikao cha Waziri wa Madini katika mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.
Baadhi ya washiriki walioshiriki kikao wa Waziri wa Madini katika mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo kwenye kikao katika mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto akiwa ameongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila mara baada ya kikao katika mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akielekea kwenye gari mara baada ya kikao katika mgodi wa Williamsoni Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akizungumza jambo kwenye kikao kilichofanyika katika mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa mgodi wa madini ya Almasi wa Wiliamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.
Na Tito Mselem ,Shinyanga
Waziri wa madini Doto Biteko amesikitishwa na kitendo
walichokifanya uongozi wa mgodi wa madini ya Almasi wa Williamson Diamond
Limited (WDL), uliopo Mwadui katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga cha
kutaka kuuza kinyemela mgodi huo bila Serikali kupewa taarifa.
Hayo yamesemwa Julai 5, 2020 na Waziri wa Madini Doto Biteko
alipofanya ziara yake kwenye mgodi huo mara baada ya kuona matangazo ya kuuzwa
kwa mgodi huo kwenye mitandao ya kijamii.
Waziri Biteko, alisema Serikali inaubia wa asilimia 25 katika
mgodi wa WDL, haiwezekani utakekuuzwa bila mmbia wake kufahamu kitendo hicho ni kukiuka taratbu na Sheria za
nchi.
“Serikali inaubia wa asilimia 25 kwenye mgodi huu kama mnataka
kuuza mgodi lazima mtoe taarifa serikalini na mpate kibali, kwa mantiki hiyo
serikali inapaswa kuwaadhibu kwa kutaka kuuza mgodi bila kibali huko ni
kuhujumu nchi,hivi mlituuliza serikali hatuna uwezo wa kununua mgodi na
kuuendesha?,” alisema Waziri Biteko.
Kutokana na kitendo hicho, Waziri Biteko ameuagiza uongozi wa
mgodi huo kufikia Julai 10 mwaka huu wawe wametoa maelezo kwa maandishi kueleza
sababu za kutaka kuuza mgodi huo bila mmbia wake ambaye ni Serikali kujua na
pia, kutoa taarifa ya kuwapunguza kazi wafanyakazi kisha kuwalipa nusu
mshahara.
Alisema wafanyakazi waliopunguzwa kazi kwa kutumia kigezo cha
ugonjwa wa Corona utaratibu uliotumiwa haufai na wao kama Wizara ya Madini
hawakubaliani nao kutokana na kulipwa mishahara nusu jambo ambalo linawapa wakati
mgumu na kusababisha migogoro isiyo ya lazima.
Aidha, Waziri Biteko, alisema sababu ambazo wanazitoa mgodi huo
za kusitisha shughuli za uzalishaji na kutaka kuuza mgodi huo ni kushuka kwa
bei ya almasi duniani iliyosababishwa na ugonjwa wa corona, ambapo alieleza kuwa
sababu hizo hazina mashiko ila wawe wakweli kama wamefilisika ijulikane.
Waziri Biteko alisema sababu kubwa ambayo ingefanya mgodi huo
kufungwa ni kushuka kwa uzalishaji na siyo uendeshaji, huku akihoji kama mgodi
hauna fedha za kujiendesha wangesema badala ya kuweka matangazo kwenye mitandao
mgodi unauzwa wakati serikali haina taarifa.
kwenda mitandaoni.
Kwa upande wake meneja mkuu wa mgodi huo Mhandisi Ayoub Mwenda,
alikiri kuwa hawakutoa taarifa Serikalini juu ya kutaka kuuzwa kwa mgodi huo,
huku akieleza kuwa walifunga mgodi huo April 8 mwaka huu kutokana na kushindwa
kujiendesha na ameahidi kufuata maelekezo yote ambayo yametolewa na Waziri wa Madini.
Mhandisi Mwenda alisema walikuwa wanazalisha vizuri kabla ya
mlipuko wa ugonjwa wa Corona ambapo kwa mchanga waliokuwa wameuzalisha walikuwa
mbele kwa asilimia tatu na almasi walizokuwa wamezikusanya walikuwa mbele kwa
asilimia 9.1kulingana na bajeti yao waliyokuwa wameiweka.
Alisema tatizo la Corona limeuathiri sana mgodi huo na kusimama
kufanya shughuli za uzalishaji kutokana na kushuka bei ya masoko ya nje ambapo
kabla ya Corona bei ilikuwa dola 246 kwa karati moja ambapo Machi mwaka huu
waliuza karati moja dola 135 ambayo ilikuwa haiwezi kutosheleza gharama za
uzalishaji.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba ameipongeza Wizara
ya Madini kwa kazi nzuri wanazozifanya ambapo wamesaidia nchi kuingia katika
uchumi wa kati.
Social Plugin