Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dkt. Abdallah Jacobo Seni akionesha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini leo Julai 16,2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dkt. Abdallah Jacobo Seni amechukua fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini leo Julai 16,2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Dkt. Abdallah Jacobo Seni ambaye ni mhadhiri wa masuala ya Elimu alichukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia mwaka 2010 na 2015 na mwaka huu itakuwa ni awamu ya tatu kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Amesema bado hajakata tamaa kuomba kupeperusha bendera ya CCM akibainisha kuwa huenda sasa wananchi wa Shinyanga wameelewa dhamira yake ya kuwatumikia kwa kuwaletea maendeleo na kutatua kero zao.
“Hii ni mara ya tatu nachukua fomu kuomba CCM inipe ridhaa ya kuwa mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini. Mimi sikati tamaa kwani naamini huenda sasa ni zamu yangu kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini”,amesema Dkt. Seni.
Akizungumza na Malunde 1 blog, Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu amesema hadi kufikia leo Julai 16,2020 majira ya saa 10 jioni, jumal a wanachama 53 wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu kuomba kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Amesema leo Julai 16,2020 wanachama watano wamechukua fomu ambao ni Mhima Stephen Singu, Rebecca Daudi Kahema,Khamis Bakari Maganga, Amri Karanda Risasi na Abdallah Jacobo Seni na kufanya idadi kuwa 53 tangu zoezi la uchukuaji fomu lilipoanza Julai 14,2020.
Social Plugin