Rais mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa enzi za uhai wake akizungumza na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere enzi za Uhai wake.
Na Janeth Raphael Michuzi Tv
HAKIKA usiku wa kuamkia leo Julai 24,2020 utakuwa usiku wa kukumbukwa daima katika mioyo ya Watanzania na hata nchi nyingine nyingi ulimwenguni kutokana na taarifa za kifo cha Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye enzi za uhai wake alikuwa kiongozi mahiri, kiongozi aliyesimamia misimamo yake na asiyekuwa wa kukata tamaa.
Ilikuwa ni majira ya takriban saa 6 na nusu usiku ambapo Rais wetu mpendwa Dk.John Pombe Magufuli alipotangaza kifo cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Wakati taarifa hizo zinatolewa Watanzania wengi walikuwa wameshalala. Hata hivyo taarifa hizo za kusikitisha zilisambaa kama upepo na kuleta majonzi kwa Watanzania wote kwa kuodokewa na Rais huyo mstaafu aliyehakikisha anaijengea heshima nchi yetu katika uso wa Dunia.
Hakika Rais mstaafu Benjamin Mkapa atakumbukwa kwa mengi aliyoyafanya hapa nchini na hata nje ya nchi ukiwepo ushirikiano wake katika kuleta amani kule kwa majini zetu Kenya kutokana na machafuko ya kisiasa wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2017-2018.
Yapo mengi ya kukumbukwa kutoka kwa kiongozi huyu shupavu, hata yakiandikwa hapa hayataisha. Ila kwa wanamichezo pia hawatakusahau kwa kusimamia kidete suala la ujenzi wa kisasa wa Uwanja wa Mpira pale Taifa. Ukweli Baba umeacha alama kubwa sana.
Tangulia Baba njia yetu ni moja tutaonana Tena.
Social Plugin