Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMOSY MSHANDETE ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SOLWA

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Ernestina Richard akimpatia fomu ya kuomba kugombea ubunge Amosy Malugu Mshandete.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Amosy Malugu Mshandete amechukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga.

Mshandete amechukua fomu leo Jumanne Julai 14,2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu,Mshandete ameamua kuomba ridhaa ya CCM agombee ubunge kwani amejitathmini na kuona kuwa anao uwezo wa kutoa mchango wa maendeleo katika Jimbo la Solwa kwa kushirikiana na wananchi na serikali.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Ernestina Richard akimpatia fomu ya kuomba kugombea ubunge Amosy Malugu Mshandete.
 Amosy Malugu Mshandetete akionesha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga.
 Amosy Malugu Mshandetete akionesha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com