NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jumuiya za Watumia Maji Mto Pangani chini uliofanyika kwenye viwanja vya Sokoni wilayani Pagani |
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah akizungumza wakati wa uzinduzi huo
KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso katikati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jumuiya ya Watumia Maji Mto Pangani chini na ugawaji wa vitendea kazi kwa Jumuiya kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Bonde la Maji Mto Pangani Dkt Victor Runyoro na kulia ni Mkurugenzi wa Bonde la Maji la Mto Pangani Segule Segule
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akijaribu moja ya vitendea kazi vilivyotolewa kwa Jumuiya ya watumia maji Mto Pangani chini wakati alipoizindua
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo
Sehemu ya vifaa walivyokabidhiwa
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso amezindua Jumuiya ya watumiaji wa Maji Mto Pangani chini wilayani Pangani huku akizitaka vifaa vilivyokabidhiwa kwa ajili ya kufuatilia rasilimali za maji wasivitumie kama bodaboda na kupakiza nazi badala yake vitumike kwenye matumizi yaliyokusudiwa.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya Watumiaji Maji wa Mto Pangani chini katika halfa iliyofanyika mjini humo na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani Dkt Victor Runyoro na Mkurugenzi wa Bonde la Maji la Mto Pangani Segule Sugule.
Alisema kwamba kumekuwa na tabia jumuiya zinapokabidhiwa vifaa kwa kufuatilia rasilimali za maji huacha kufanya hivyo huku wakivitumia kwenye matumizi ambayo hayajakusudiwa huku akitoa onyo kwao.
“Ndugu zangu mmekabidhiwa vifaa hivi ikiwemo pikipiki hivyo niwatake isije kutokea bodaboda zikaenda kupakizwa nazi na popoo na kuacha kutumika kwenye matumizi yaliyokusudiwa kwani kufanya hivyo mtakuwa hamtendi haki na tutakaowabaini tutawachukulia hatua “Alisema Naibu Waziri Aweso.
Hata hivyo alisema kwamba anaamini vifaa hivyo ambayo vimetolewa vitakuwa chachu kubwa katika jumuiya hizo kuhakikisha zinaweza kushughulikia changamoto mbalimbali.
Aidha alisema kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni lazima wahakikishe wanatimiza majukumu yao na waledi mkubwa ili kuweza kuongeza ufanisi wakati wakitekeleza majukumu yao.
“Ndugu zangu wajibu wenu ni kuhakikisha mnasimamia ipasavyo rasilimali za maji kutokana na uwepo wa vitendea kazi hivyo mimi ni kijana wenu ikitokea mnafanya vibaya tutaivunja na kutafuta watu wengine ambao wataweza kufanya kazi kwa mujibu wa katiba iliyoasisiwa”Alisema
Hata hivyo aliwaambia kwamba yeye ni kiongozi kutoka wilayani humo hivyo laqzima wahakikishe wanakuwa jumuiya ya mfano hapa nchini kwa kufanya kazi kwa waledi mkubwa.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri Aweso Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani Dkt Victor Runyoro alisema bonde la Pangani linasimamia wilaya 20 ambazo ni nyingi lakini kwa majukumu waliopewa kisheria na kubwa ni kuhifadhi rasiliamali maji.
Alisema kwamba maeneo mengi wanamatatizo ya maji wanapata shida sana na jinsi idadi ya watu inavyozidi kuongezaka maji kwa mtu mmoja yanadizi kupungua.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Bonde la maji la Mto Pangani Segule Segule alisema suala la utunzaji wa maji ni jukumu lao kila mmoja kuhakikisha rasilimali za maji vinatunzwa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo
Alisema uundwaji wa jumuiya hizo zinaundwa kwa kuzingatia sheria za rasiliamali za maji ya namba 11 ya mwaka 2009 katika maelekezo ya sheria kuunganisha maelezo ya sera ya maji 2002 ambayo inataka ushirikishwaji jamii kwenye miradi na masula yote yanayohusu maji.