Musa Jonas Ngangala akionesha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
*****
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Musa Jonas Ngangala amechukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Musa Jonas amewasili katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumanne Julai 14,2020 majira ya saa tatu na kuchukua fomu ya kuomba kugombea ubunge katika Jimbo la Shinyanga.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Musa Jonas Ngangala ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Imalilo kata ya Kitangili katika Manispaa ya Shinyanga mwenye Elimu ya Shahada ya Mipango Miji na Maendeleo amesema endapo chama chake kitampa ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini atahakikisha anasimamia na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kikamilifu ikiwa ni pamoja na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
"Nimechukua fomu ili kuomba ridhaa chama changu kinipatie nafasi ya kwenda kuwatumikia wananchi,naamini chama changu kikinipitisha kugombea Ubunge nitakuwa mwakilishi mzuri wa wananchi katika kutatua kero za wananchi na kutekeleza miradi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi",amesema Ngangala.
Musa Jonas Ngangala akinawa mikono baada ya kuwasili katika ofisi cha CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kuchukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Social Plugin