Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa NEC Salim Abri Asas akitoa nasaha kwa wagombea ambapo alisema kuwa chama hakina mgombea maalum bali wagombea wote wapo sawa na watapita katika mchakato wa kikanuni ili kumpata mgombea mmoja atakayepigiwa kura na wajumbe.
Na Zuhura Zukheir - Malunde 1 blog Iringa
Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimetoa onyo kali kwa wagombea ubunge na udiwani kuwa hakitawafumbia macho wagombea wote watakaobainika kusaliti chama kwa kukiuka kanuni na taratibu za chama baada ya uchaguzi wa kura za maoni kumalizika na kupatikana mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano na wagombea wa nafasi za ubunge katika kikao cha maelekezo kuelekea kura za maoni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa Dkt. Abel Nyamahanga alisema kuwa katika kuelekea uchaguzi wagombea wanatakiwa kuwa na moyo wa ujasiri kwani lolote linaweza kutokea na wasipojiandaa wanaweza kuangukia katika usaliti jambo ambalo sio jema kwa watu walioaminiwa na chama.
Alisema katika uchaguzi wanatarajia kuona wagombea wote waliojitokeza katika majimbo saba ya uchaguzi na kata kata 106 za udiwani wataunganisha nguvu zao kuhakikisha ushindi wa kishindo unakuwaCCM hata kama wao watakuwa wamekatwa majina yao.
"Kila mgombea anatakiwa kutambua kuwa katika uchaguzi kuna kupata na kukosa hivyo hatutegemei baada ya kura za maoni kujitokeze masuala ya usaliti na makundi ya wagombea",alisema.
Aliwataka wagombea kutambua kuwa masuala ya usaliti yamekuwa yakikigawa chama na kusababisha wapinzani kupata nguvu ya kuchukua majimbo jambo ambalo halikubaliki katika uchaguzi wa mwaka huu katika chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa nafasi ya ubunge waliyoomba ni ya utumishi hivyo ni vyema wakajitoa kwa moyo kuwatumikia wananchi na wanaccm kwa ujumla badala ya kufikiria kupata utajiri kupitia ubunge.” Wagombea ni waeleze hakuna mgombea ambaye yupo juu zaidi ya mwingine wagombea wote wapo sawa hata wale wabunge wanaotetea nafasi zao wote kwa sasa ni wanachama tu wa kawawida.
Alisema kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi kuna miongozo ya kikanuni kwa watia nia pamoja na viongozi wa chama hicho ambayo ni mwiko kwa kiongozi yeyote kupendelea mgombea au mtia nia yeyote wa
Aliongeza kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi kina nia njema na wagombea wote hivyo wanatakiwa kujenga imani na chama chao na hata ikitokea mmoja amepitishwa wengine wa muunge mkono ili kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo.
Aidha alisema chama hakitamvumilia mgombea yoyote atakaye mchafua mgombea mwingine kwa kuwa haijulikani jina lipi litarudishwa hivyo ikitokea mgombea aliyechafuliwa akapitishwa chama kinapata wakati mgumu kumsafisha kipindi cha kampeni.
Nyamahanga pia amewataka wagombea kumtegemea Mungu zaidi badala ya kupishana kwa waganga wakienyeji ambao ndio wamekuwa chanzo cha migogolo katika chama baada ya kuwahakikishia ushindi baadae mambo yanakuwa tofauti.
Akizungumza Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa NEC Salim Abri Asas alisema kuwa chama hakina mgombea maalum bali wagombea wote wapo sawa na watapita katika mchakato wa kikanuni ili kumpata mgombea mmoja atakaepigiwa kura na wajumbe.
Alisema kuwa anaamini katika mchakato huo wa kura za maoni hakutakuwa na manung’uniko kwani kura zitapigwa za wazi na kila mgombea atahusika katika kuhesabu kura ili kuondoa malalamiko.
MNEC Asas aliwaomba watia nia kuunganisha nguvu zao kumsaidia atakaepitishwa nchama baada ya uchaguzi wa kura za maoni ili kuhakikisha wanapata ushin za di wa kishindo pamoja na kupata ushindi wa kishindo katika kura za Rais mh. John Magufuli.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa Brown Mwangomale aliwataka wagombea kujiandaa kisaikolojia katika mchakato wa uchaguzi na wa kubali matokeo kwakuwa katika uchaguzi kuna matokeo mawili ambayo ni kushinda na kushindwa.
Alisema kuwa kitendo cha kujiamini katika uchaguzi wa kura za maoni kuwa utashinda na badala yake matokeo ya kawa tofauti ndipo wanachama wanapogeukia katika usaliti jambo ambalo halikubaliki katika chama.
Alisema kuwa dhambi ya usaliti ni mbaya na adhabu yake kufukuzwa katika chama jambo ambalo halitarajiwi kujitokeza katik uchaguzi huu wa mwaka 2020”ndugu zangu dhambi ya usaliti ni mbaya na kubwa usaliti unaua na ndio maana vitabu vya dini vimekemea vikali usaliti.
Alisema kuwa CCM mkoa wa Iringa wamedhamiria kushinda katika majimbo yote ya uchaguzi hivyo ushindi huo unatemewa zaidi na mshikamano utakaoneshwa na mshikamano wa wagombea wote 319 walioingia katika kuwania nafasi hiyo ya ubunge.
UBUNGE WA JIMBO
Mwangomale alisema aliojitokeza kugombea Jimbo la Iringa Mjini 54,Isimani 9,Kalenga 68, Kilolo 38, Mufindi kusini 31 na Mufindi Kaskazini 33,Mafinga Mjini 20,Ubunge Viti maalumu 28,Jumuiya ya vijana 13, Jumuiya ya wazazi 8,Kundi la Wafanyakazi 4,kundi lawatu wenye ulemavu 5 na Kundi la wasomi 3.
UDIWANI
Walitokeza kugombea ngazi ya udiwani kwa kata 106 za mkoa wa Iringa kutia nia ngazi ya udiwani 787 ammbapo katika kata za Iringa mjini wamejitokeza 148,Wilaya ya Iringa 156,Wilaya ya Mufindi 171 pamoja na kilolo 117.
Mwangomale aliongeza kuanzia jumatatu julai 20 hadi jumatano kutakuwa na mchakato wa kura za maoni kila wilaya za kuwapata wagombea watakaopeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa NEC Salim Abri Asas akitoa nasaha kwa wagombea
Social Plugin