Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU.....AWATAKA WAKACHAPE KAZI KWA BIDII

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka viongozi wapya walioapishwa leo kuimarisha ushirikiano mzuri na watendaji waliopo katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza ufanisi mzuri katika utendaji kazi wa kuleta maendeleo ya kujenga nchi.


Wito huo ameutoa leo Ikulu ya Jijini Dodoma wakati wa kuwaapisha viongozi wapya walioteuliwa hivi karibuni.

Aidha Rais Magufuli, amesema kuwa ufanisi mzuri wa watendaji hao katika nafasi zao ndio itakuwa chachu ya kuendelea kuinua uchumi wa kati kutoka hapo ulipo na kukua zaidi.

“Nendeini mkachape kazi ya kuwatumikia watanzania kwa kumtanguliza Mungu ili kuweza kufanikiwa katika kutekeleza majukumu yenu”, amesisitiza Rais Magufuli. (PICHA: IKULU)


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com