Sherehe kama hizi za ligi ya mabingwa hazitoruhusiwa leo kwa Liverpool
Polisi ya Merseyside imeonya mashabiki wasikusanyike nje ya uwanja kwa kudhani Liverpool italitembeza kombe la ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.
Polisi ya Merseyside imeonya mashabiki wasikusanyike nje ya uwanja kwa kudhani Liverpool italitembeza kombe la ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.
Liverpool inashuka uwanja wao wa nyumbani Anfield usiku huu, kuikaribisha Chelsea, na mchezo huo, utakuwa wa kukabidhiwa ubingwa wa EPL walioukosa kwa miaka 30.
Polisi imeandika kwenye twita kuwa kuna upotoshaji kuwa wachezaji wa Liverpool watatoka nje na kombe kusherehekea na mashabiki.
"Uzushi umezagaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu timu kuwa itatoka nje ya uwanja wa Anfield usiku wa leo.
"Kwa asilimia 100% haitotokea.Sehemu pekee ya kuangalia sherhe za ubingwa ni kwenye TV. Tafadhari sikilizeni ushauri wa kocha na wachezaji wenu. Hivi ndivyo wanavyotaka.''.Ilisema taarifa hiyo.
Polisi imethibitisha kutakuwa na dolia kuzunguuka uwanja kipindi chote cha mchezo huo hadi utakapoisha.
Marufuku ya mikusanyiko inaendelea nchini Uingereza huku nchi hiyo ikiendelea kupambana na maambukizi ya COVID-19.
Hivi karibuni Serikali ya Uingereza kupitia Waziri Mkuu wake Boris Johnson ilitangaza kuwa inafikiria kulegeza vizuizi vya watu kukusanyika na itafungulia mashabiki kuingia kwenye viwanja vya soka kuanzia mwezi wa Oktoba mwaka huu.
Social Plugin